Baada ya Gigy Money kumkana mpenzi wake wa zamani 'Mo J' na kudai kuwa anatoka na Joti, leo Joti amkana Gigy Money live
Gigy Money amekuwa akimpost mchekeshaji Joti na kufuta picha za mpenzi wake Mo J, mwanzoni mwa wiki hii Gigy aliulizwa kwenye YOU HEARD na kudai kuwa Joti mdiye mpenzi wake wa sasa na kuthibitisha kuachana na Mo J
Leo katika kipindi cha XXL clouds FM, Sudy Brown kwenye YOU HEARD amepiga stori na Joti kuhusu swala hilo, haya yalikuwa majibu ya Joti
‘Mimi kwa heshima ambayo nimeitengeneza na watu wangu ninaofanya nao kazi halafu wewe unataka kuiharibu kwa mara moja, huyo Gigy unayemzungumzia picha ambazo amepost umeona picha ambayo mimi nafanya nae mapenzi?”
“Mimi siilewi…………mimi nina mke wangu, nina familia yangu, mbona unataka kuniweka kwenye maisha ambayo wanaishi watu, mimi siishi huko’
No comments: