Header Ads

Karibu ndugu msomaji katika makala hii inayohusu namna ambavyo kijana anapaswa kuishi ujana wake ili kujiwekea uhakika wa maisha mazuri hapo baadae. Kutokana na maendeleo ya sayansi na tekinolojia kumewafanya vijana wengi kuwa wavivu wa kufikiria, wavivu kujifunza na kushindwa kujiongoza wenyewe jambo ambalo limewasababishia vijana wengi kujiingiza kwenye makundi mabaya kama ya walevi, watumia madawa ya kulevya na makundi mengine ya uhalifu kama wizi na ujambazi ambapo mwishowe huwa mbaya na kufanya kijana ashindwe kutimiza malengo yake.
Kijana anaejielewa anatakiwa kuishi kwa namna ambayo atakua unaiona kesho yake japokuwa hatuna uhakika wa kufika kesho ila sio sababu ya kuishi bila dira, angalau unapaswa kuwa na taswira kidogo kuhusu kesho yako. Zingatia mambo yafuatayo ili kujenga kesho nzuri na imara.

1 Uwezo wa kujiongoza mwenyewe.
  Kijana yeyote anayejielewa huwa na uwezo wa kujimiliki mwenyewe pasipo kuendeshwa na influence zisizokuwa na faida, kwanza tambua baya ni lipi, jema ni lipi, chenye faida ni kipi na kisicho na faida ni kipi kisha chagua mwenyewe cha kufanya. Unatakiwa kuishi kwa kufuata mikakati uliyojiwekea ili kutimiza malengo yako, vinginevyo utayumbishwa na mambo yasiyo na faida kwenye maisha yako na kujikuta ukipoteza malengo uliokuwa umejiwekea, kumbuka kila mtu ana malengo yake tofauti na ya kwako na kila mtu anatoka familia tofauti na ya kwako.

2 Imani.
  Hapa haijalishi wewe upo katika imani gani, dini gani au dhehebu gani, imani itakusaidia kuishi katika maadili na nidham hii itafanya jamii ikuamini na hii itakupa michongo kibao ya kazi  na kupata mke/mme anayeeleweka. Imani pia husaidia sana katika kufanikisha mambo mengi, kumbuka zamani babu zetu waliiomba  miti na mvua zikanyesha.

3 Chagua malengo yako kisha jiwekee mikakati ya kuitimiza.
  Wengi tumekuwa  na malengo lakini tumekuwa tukifikiri labda muda wa kutimiza malengo hayo haujafika, asikudanganye mtu hakuna maisha mengine tofauti na haya "wakati wako ndio leo kutimiza malengo yako" jiwekee leo mikakati ambayo utaanza kuizingatia leo katika safari ya kutimiza malengo yako.

4 Penda kujifunza na kuwa updated kwa habari na matukio ya kila siku.
  Kuna njia nyingi za kujifunza ila kubwa ni kusoma vitabu na makala mbali mbali, kijana haupaswi kuwa na mipaka katika kujifunza hakikisha kila siku unaingiza kitu kipya kichwani, penda kusoma vitabu soma magazeti pia, penda kusikiliza hotuba za viongozi mbali mbali hasa wazamani na mafundisho ya kidini. Hii itakusaidia kuelewa mambo mengi yatakayo kufanya ujiamini na kutambua njia sahihi ya kupita.

5 Kuwa na mpenzi mmoja.
  Yale maswala ya kuwa na michepuko millioni  sikuhizi yamepitwa na wakati, unakuta kijana una miaka 22 bado una madem kibao, utachelewa huo ni muda wa kufanya mambo ya msingi na sio kuwaza tena wanawake watakurudisha nyuma, tumia muda wako mwingi kuwaza maendeleo na kubuni njia ambazo utazitumia kuongeza kipato chako, unashauriwa kuwa na mpenzi au mchumba mmoja.

6 Matumizi ya Fedha. Nidhamu ya fedha ni jambo muhimu sana kwa kijana anayependa kufanikiwa katika maisha, jifunze tabia ya kujiwekea akiba na usiwe na matumizi yanayozidi mapato yako sio unakuwa na njia moja ya kuingiza kipato halafu njia 20 za kutumia.

7 Kuwa mtanashati na tumia Lugha ya nidhamu kwa watu wote. Nimuhimu sana kwa kijana kuwa mtanashati mudawote, hii itakusaidia kujiamini popote pia, itakusaidia kupata michongo mbali mbali na kupata marafiki wanaojielewa na hii itakusaidia sana kwasababu sikuhizi kuwa na washkaji ndio mpango mzima hasa wanaojielewa.

No comments:

Powered by Blogger.