Header Ads

MWIKA; Ajali yaua watano wakiwemo viongozi na waandishi wa habari

 

Watu watano wafariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria waandishi wa habari na baadhi ya Viongozi wa UVCCM Wilayani Moshi kupata ajali maeneo ya Mwika mkoani kilimanjaro jioni hii na kusababisha vifo vya watu watano huku wengine wakijeruhiwa vibaya.

Taarifa za awali zinasema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni FUSO kuligonga kwa nyuma gari hilo na kusababisha vifo hivyo na majeruhi.
Imeelezwa kuwa watu hao pamoja na makada wa CCM Moshi walikuwa wakitokea Wilaya ya Rombo ambako palikuwa na maadhimisho ya miaka 40 ya CCM ngazi ya Mkoa yaliyofanyika katika ukumbi wa Sekomdari ya Shauri Tanga wilayani Rombo.

No comments:

Powered by Blogger.