Mvua Ya Mawe Mkoani Tabora, Waathika Wahitaji Msaada
Mvua hii imeleta hali ya sintofahamu hapa katika kata ya Itundu wilayani Urambo ambapo zaidi ya hekta 382 za mahindi, hekta 92 za tumbaku zimeharibiwa vibaya na pia madarasa matatu na maabara ya shule ya msingi Itundu , zahanati, nyumba za walimu na nyumba za ibaada zimeezuliwa.
Hata hivyo serikali wilayani Urambo haijawatupa wananchi hawa na hapa baadhi ya viongozi wanaeleza jitihada zao katika kuwasaidia wananchi waliopatwa na maafa
Mkuu wa mkoa wa Tabora AGGREY MWANRI ambae pia amefika kujionea hali hiyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha masika.
Mvua hii iliyonyesha kwa takribani dakika kumi tu imesababisha madhara makubwa ambapo watu tisa wamejeruhiwa.

No comments: