Kamanda Sirro: Wema Sepetu, Nyandu Tozzy, TID Babuu wa kitaa bado wanashikiliwa na jeshi la polisi
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa bado wasanii hao Wema Sepetu, Dogo Hamidu, Khalid Mohamed (TID), na mtangazaji maarufu wa Clouds TV Babuu wa Kitaa bado wanashikiliwa na jeshi hilo.
“Bado tunawashikilia kwa mahojiano zaidi,” amesema Sirro kwa kifupi.
Wasanii wengine waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambao wanatakiwa kufika kituoni Jumatatu ni Vanessa Mdee, Tunda na watu wengine Halidali Kavila, Amani, Kashozi na Omry Sanga.


No comments: